Kanuni za ulinzi wa data

a) faragha

Kila anayekusanya au kutumia data binafsi lazima azingatie faragha/usiri wa mwenye data.

b) sheria

Kila anayekusanya au kutumia data binafsi anapaswa kuzingatia usheria, usawa nauwazi anapochakatua data hiyo.

c) madhumuni

Data binafsi lazima ikusanywe kwa madhumuni maalum na kwa malengo halali na isitumike kinyume cha na madhumuni hayo.

d) kupunguza

Data binafsi ikusanywe kulingana na madhumuni ya utumizi wake na isizidi madhumuni yake. 

e) ufafanuzi

Wanaokusanya data binafsi lazima watoe maelezo halali wakati wowote data kuhusu familia au mambo ya kifaragha yanahitajika.

f) sahihi

Kila hatua ichukuliwe kuhakikisha kwamba data binafsi inayokusanywa na kutumika ni sahihi, na inasasishwa au kusahihishwa bila kupoteza muda.

g) uhifadhi

Data binafsi isiwekwe kwa muundo unaomtambulisha mwenye data wakati madhumuni ya kukusanya data hiyo yamekamilika.

h) uhamisho nje ya nchi

Data binafsi isihamishwe nje ya nchi ya Kenya bila dhibitisho kwamba nchi hiyo nyingine ina sera sambamba za kutosha ulinzi wa  data binafsi, au kwa ruhusa ya mwenye data.

 

Image by freepik

Stay Updated

Subscribe to our newsletter to receive the latest research, publications, and blog posts directly in your inbox.